Msako mkali dhidi ya makanisa ya kikristo umeanza China na kuzua taharuki

In Kimataifa

Hatua ya hivi karibuni ya msako mkali unaotekelezwa na polisi dhidi ya makanisa nchini China umesababisha taharuki kubwa kwamba serikali ya nchi hiyo inaonesha ubabe wake wa kuwakandamiza Wakristo.

Miongoni mwa waliokamatwa ni kasisi mmoja maarufu pamoja na mkewe. Wote ni wamiliki wa kanisa la Early Rain Covenant lililoko katika jimbo la Sichuan. Wawili hao wanashtakiwa kwa kosa la kuhujumu utendakazi wa serikali ya kikomunisti ya China na kwenda kinyume na maadili ya Wachina.

Juamamosi asubuhi, kikosi cha polisi kilivamia darasa moja la kidini lililokuwa likiwapa mafunzo watoto ndani ya kanisa la Rongguili huko Guangzhou.

China ni nchi isiyomuamini Mungu, japo mamlaka zinazesa zinatoa uhuru wa kuabudu.

Lakini kwa miaka mingi utawala wa nchi hiyo umechukua hatua dhidi ya viongozi wa kidini, ambao wanaonekana kutishia mamlaka au kuyumbisha uongozi wa taifa, ambayo kwa mjibu wa shirika la Human Rights Watch, “”Hufanya kejeli kwa madai ya serikali kwamba inaheshimu imani za kidini”.

Serikali inawashinikiza wakristo kujiunga na mojawepo ya makanisa makubwa matatu inayoonyesha uzalendo kwani zimepigwa msasa na serikali pamoja na chama tawala cha Kikomunisti, huku yakiongozwa na makasisi walioidhinishwa na serikali.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MBUNGE JAGUAR WA KENYA ALIYETISHIA KUWAFURUSHA WATANZANIA AKAMATWA

Maafisa wa polisi nchini Kenya wamemkamata mbunge wa jimbo la Starehe anayedaiwa kutoa kauli za chuki dhidi ya wafanyabiashara

Read More...

MANCHESTER CITY, YAMTOA KAFARA DANILO

. . Klabu ya Manchester City, ipo tayari kutoa kiasi cha paundi milioni 44 na beki wao wa pembeni

Read More...

TOTTENHAM MBIONI KUMSAJILI KIUNGO KUTOKA LYON.

. . Klabu ya Tottenham, imekubali kutoa kitita cha kiasi cha paundi milioni 62 kumsajili kiungo wa kati wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu