ACT Wazalendo, CHADEMA waungana.

In Siasa

Vyama vya upinzani ACT Wazalendo na CHADEMA vimeafikiana kuweka mgombea mmoja wa Ubunge anayekubalika katika jimbo la Buyungu ili kurudisha jimbo hilo mikononi mwa upinzani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kiongozi wa ACT Wazalendo, Mhe. Zitto Kabwe amesema kuwa makubaliano hayo yameafikiwa pia na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe. Freeman Mbowe ambapo kwa pamoja wataangalia mgombea mwenye ushawishi zaidi katika jimbo hilo iwe kutoka ACT Wazalendo au CHADEMA na kumuweka kuwa mgombea rasmi wa ubunge.

Kwa heshima ya Mwalimu Bilago Mimi na Freeman Aikaeli Mbowe tumekubaliana kuwa tutashawishi kuwepo na a Democratic Front Katika Jimbo la Buyungu. Ama Act Wazalendo itaunga mkono mgombea wa CHADEMA au CHADEMA itaunga mkono mgombea wa ACT Wazalendo. Tunataka kuweka mgombea mmoja anayekubalika na Wananchi wa Buyungu na kufanya kampeni kwa pamoja mpaka ushindi.“amesema Zitto Kabwe na kueleza lengo la kufanya hivyo.

Huu ni mwanzo wa harakati za kuwa na United Democratic Front dhidi ukandamizaji wa Demokrasia nchini na dhidi ya Hali mbaya ya Maisha ya Watu wetu. Umoja wa zaidi ya vyama vya siasa ukihusisha Vyama vya Wafanyakazi, Vyama vya Wakulima, Vyama vya Wafanyabiashara na Wananchi wengine.“amemaliza Zitto.

Jimbo la Buyungu kwa sasa lipo wazi baada ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo kupitia tiketi ya CHADEMA, Kasuku Samson Bilago kufariki dunia mnamo Mei 25, 2018 .

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Mwanamfalme Saudia Kuchunguzwa kifo cha Khashoggi.

Kuna ushahidi kamili kwamba mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman na maafisa wengine wa ngazi za juu wanahusika kibinafsi

Read More...

Hafla ya kutambulisha tuzo ya serengeti yafanyika.

Waziri wa maliasilai na utalii Mh Hamis Kigwangala leo ameshiriki katika zoezi la utambulishwaji wa Tuzo ya Mbuga ya

Read More...

Serikali inadaiwa zaidi ya bilioni 6.

Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza kupitia Jeshi hilo limeiomba Serikali kuwalipa deni la shilingi Bilioni 6.45 fedha zilizotumika

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu