Afariki Dunia baada ya kufukiwa na kifusi 

In Kitaifa

Mtu mmoja amefariki Dunia na wengine Wanane wameokolewa, baada ya kufukiwa na kifusi katika machimbo ya dhahabu ya Shilalo yaliyopo kwenye kata ya Inonelwa wilayani Misungwi mkoani Mwanza.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mwanza, – Jumanne Muliro amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa vikosi vya uokoaji vinamtafuta mtu mwingine ambaye anadhaniwa bado amenasa katika kifusi hicho.

Kamanda Muliro amesema kuwa, tukio hilo limetokea saa Saba usiku wa kuamkia hii leo, ambapo watu hao Kumi waliingia katika machimbo hayo kwa ajili ya kufanya kazi zao za uchimbaji kama kawaida.

Amesema kuwa, mara baada ya kuingia kwenye machimbo hayo, kifusi kiliporomoka na kuwafukia ambapo jitihada za uokoaji zilianza mara baada ya tukio hilo.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tetesi za soka Ulaya.

Inter Milan wanafikiria kumnunua kiungo wa kati, Mfaransa N'Golo Kante huku Blues wakiwa tayari kusikiliza ofa kwa ajili

Read More...

Manchester City kushiriki kombe la Ulaya.

Klabu ya Manchester imefanikiwa kubadili marufuku ya miaka miwili kushiriki katika mashindano ya klabu bingwa Ulaya kuanzia msimu

Read More...

Mama akiri kuua Watoto wake wanne.

Mwanamke mmoja nchini Kenya Betrice Mwende, anayeshikiliwa kwa tuhuma za kuwaua watoto wake wanne, amekiri Mahakamani kuwa ni

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu