Ajira za wazawa kulindwa.

In Kitaifa

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema serikali inadhibiti raia wa nje wasipate ajira kwenye maeneo ya usalama kama bandari, viwanja vya ndege na mipakani ili kulinda usalama wa nchi.

Sambamba na hilo, amesema Wakala wa Barabara nchini (Tanroads) na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (Tarura), wameanza ukarabati wa miundombinu ya barabara na madaraja yaliyoharibika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini. Akizungumzia ajira za wageni katikia maswali ya papo kwa hapo bungeni jana, Majaliwa alisema; “Kwa sasa tunaendelea kudhibiti maeneo hayo ya usalama na hakuna mgeni anafanya kazi huko.

“Hata ukikuta mgeni ameajiriwa na kampuni, basi jua kuwa kutakuwa hakuna Mtanzania kwenye sifa ya kazi anayoifanya, tunasimamia sana hili hakuna ujanjaujanja.” Alisema ajira za wageni zimeruhusiwa katika nafasi za kitaaluma tu ambazo Watanzania hawana utaalamu nazo. Hata hivyo alisema katika taasisi moja inaruhusiwa kuwa na wageni wasiozidi watano. “Ofisi yangu inaendelea kusimamia hili ili Watanzania wapate fursa na tunadhibiti wageni wasichukue ajira hizi,” alisema.

Alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Leah Komanya (CCM) aliyetaka kufahamu kama serikali inadhibiti maeneo ya usalama wa nchi kama bandarini, uwanja wa ndege na mipakani ili wageni wasiajiriwe kwani kwa sasa kuna wimbi kubwa la wageni kupata ajira nchini. Kuhusu athari za mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini, Waziri Mkuu alisema tayari Tarura na Tanroads wameanza kukarabati miundombinu iliyoharibiwa na mvua hizo.

Alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema) aliyetaka kufahamu hatua iliyochukuliwa na serikali kurejesha mawasiliano ya miundombinu iliyoharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha, ambapo alisema baadhi ya mikoa imeshafanya tathmini ya uharibifu huo kwa miezi miwili sasa.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu