Al-Assad ashinda uchaguzi kwa asilimia 95 kura

In Kimataifa

Rais wa Syria Bashar al-Assad ameshinda muhula wa nne madarakani kwa kupata asilimia 95.1 ya kura zote zilizopigwa. Vyama vya upinzani Syria pamoja na mataifa ya Magharibi vimemkosoa Assad na kusema kwamba uchaguzi huo ulitawaliwa na udanganyifu. Serikali ya Assad imesema uchaguzi uliofanywa Jumatano unaonyesha kwamba Syria inaendesha shughuli zake kikamilifu licha ya mgogoro wa mwongo mzima. Vita hivyo vimesababisha vifo vya mamia kwa maelfu ya watu na wengine milioni 11 ambao ni nusu ya idadi ya watu kupoteza makazi yao. Spika wa bunge Hammouda Sabbagh alitangaza matokeo katika mkutano wa waandishi wa habari jana, na kusema kwamba asilimia 78 ya watu walijitokeza kupiga kura ambayo ni zaidi ya Wasyria milioni 14.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu