Alichokifanya Zitto Kabwe alipofika katika Kata yenye Diwani wa ACT Wazalendo.

In Kitaifa, Siasa

Wakazi wa kata ya Tomondo wilayani Morogoro jimbo la Morogoro Kusini Mashariki wiki hii imekuwa ni ya neema kwao kutokana na kupata ufumbuzi wa baadhi ya kero za miradi yao mbalimbali ya maendeleo.

Kata hiyo inayoongozwa na Diwani wa Chama cha ACT Wazalendo, Hamisi Msangule February 21, 2018 ilitembelewa na viongozi wa chama hicho ngazi ya Taifa, Mkoa na Jimbo ambao waliwezesha kutatua baadhi ya changamoto.

Changamoto kubwa ambayo imepewa kipaumbele kutatuliwa na chama hicho ni kero ya maji inayowakabili wakazi wa kata hiyo ambayo chama hicho kimeahidi kuwapeleka wataalamu wa kutoboa visima virefu kwenye kila Kijiji ndani ya mwezi huu.

Akizungumza kwenye kikao cha ndani na wananchi wa kata hiyo Kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe aliwaambia wananchi hao kama watashindwa kumaliza kero hiyo haitakuwa na maana tena chama hicho kupewa dhamana tena kuongoza.

“Chama chetu ni tofauti sana na vyama vingine, tunafanya siasa za maendeleo kwa ushirikishaji wananchi katika kutatua changamoto zao,” -Zitto Kabwe

Mbali ya ahadi ya kumaliza kero ya maji kiongozi huyo pia amechangia mifuko ishirini ya saruji kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa barabara inayokatiza kwenye mto Lugwa kwenye Kijji cha Vuleni.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu