Rais Magufuli alifanya mabadiliko kwa kumuondoa aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi katika nafasi hiyo Dr Mwigulu Nchemba na nafasi yake ikachukuliwa na Kangi Lugola.
Baada ya Dr Nchemba kuondolewa katika nafasi hiyo leo alikuwa jimboni kwake Iramba na kufanya mkutano na wananchi wake na kumshukuru Rais Magufuli kwa kipindi chote alichompa nafasi.
“Sina kinyongo, uongozi ni kupokezana kijiti, kama ambavyo mchezaji hufanyiwa technical sub hata kama kiwango chake ni kizuri, ndivyo hata serikalini hufanyika, nitaendelea kumuunga mkono Rais na serikali” >>> Dr Nchemba