Aliyekuwa kiongozi wa kundi la waasi la FPLC nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Bosco Ntaganda, hatimaye atatoa ushahidi wa kujitetea katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC siku ya Jumatano.

In Uncategorized

Aliyekuwa kiongozi wa kundi la waasi la FPLC nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Bosco Ntaganda, hatimaye atatoa ushahidi wa kujitetea katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC siku ya Jumatano.

Ntaganda maarufu kama “The Terminator” amekuwa akikanusha madai kuwa aliwatumia watoto wadogo kama wapiganaji na kuwatumia wanawake na wasichana kama watumwa wa kingono.

Kesi dhidi ya Ntanganda ilianza miaka miwili iliyopita mjini Hague, alipofunguliwa mashtaka ya mauaji katika jimbo la Ituri yaliyotokea kati ya mwaka 2002 na 2003.

Ntaganda mwenye umri wa miaka 43, amekanusha madai yote 13 ya uhalifu wa kivita na mengine matano ya ukiukwaji wa haki za binadamu, yaliyotekelezwa na waasi hao.

Watu zaidi ya 60,000 walipoteza maisha na wengine kuyakimbia makwao baada ya kuvamiwa na waasi hao.

Kabla ya kufikishwa katika Mahakama ya ICC, Ntaganda alijisalimisha katika Ubalozi wa Marekani jijini Kigali  nchini Rwanda mwaka 2013.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu