Aliyembaka mtawa wa miaka 71 afungwa maisha jela India

In Kimataifa

Mahakama moja mashariki mwa India imemhukumu mwanamume mmoja wa Bangladesh kifungo cha maisha jela kwa kumbaka mtawa mwenye umri wa 71 mnamo mwezi Machi 2015.

Mahakama hiyo ya Kolkata ilimpata Nazrul Islam na makosa ya ubakaji na jaribio la mauaji.

Watu wengine watano walihukumiwa jela kwa miaka 10 kwa wizi wakati wa kisa hicho mjini Ranaghat, magharibi mwa jimbo la Bengal.

Mtu mwengine wa sita alihukumiwa kifungo cha miaka saba jela kwa kuwaficha watu hao.

Bibi huyo mwenye umri wa miaka 71 alishambuliwa baada ya wezi hao kupora nyumba yake.

Wezi hao waliiba fedha na vifaa vyengine wakati wa shambulio hilo ambalo liliwashangaza watu wengi nchini India na kusababisha maandamano.

”Kile kilichomfanyikia mtawa huyo mwenye umri wa miaka 71 ni janga kwa sifa za jimbo la West Bengal ambapo Mama Teresa aliwafanyia kazi watu masikini”, jaji Kumkum Singha aliiambia mahakama iliojaa watu siku ya Jumatano.

Mtawa huyo ambaye hakutajwa jina lake kwa sababu za kisheria alifanyiwa upasuaji baada ya kitendo hicho kilichofanyika katika nyumba ya Jesus na Mary.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu