(ANC) wakanusha Kung’atuka kwa Zuma.

In Kimataifa

Chama tawala cha Afrika Kusini (ANC) kimekanusha taarifa zilizoripotiwa na vyombo vya habari kuwa rais Jacob Zuma atajiuzulu Kesho, Jumamosi na kusema taarifa hizo siyo sahihi na ni za kupotosha.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya mratibu mkuu wa chama hicho kwenye Bunge imesema, Chama cha ANC hakihusiki na taarifa kuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Cyril Ramaphosa amekiambia kikundi cha uongozi wa Bunge kuwa rais Zuma atajiuzulu Jumamosi na hatapewa kinga.

Mapema jana, vyombo vya habari vya Afrika Kusini viliripoti kuwa, Ramaphosa alikiambia kikundi cha uongozi cha Bunge kuwa kinga kwa rais Zuma siyo sehemu ya mjadala huo.

Ripoti hizo zilitolewa baada ya Ramaphosa kuwataka wananchi kutulia wakati wakijadili masuala husika na rais Zuma.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Suzan Kiwanga afukuzwa Bungeni.

Spika wa Bunge, Job Ndugai jana alimtoa nje ya bunge, Mbunge wa Mlimba, Suzan Kiwanga (Chadema) na kumtaka kutohudhuria

Read More...

Mtolea ajivua Uanachama wa CUF Akiwa Ndani ya Bunge Leo.

Mbunge wa Temeke Abdallah Mtolea, kwa tiketi ya CUF ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge na nafasi zote ndani

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu