Argentina Mabingwa Copa America mara 15

In Kimataifa, Michezo

Argentina wametwaa ubingwa wa #CopaAmérica 🏆 2021 baada ya kuifunga Brazil 1-0 kwenye fainali.

Huu ni ubingwa wa 15 kwa Argentina katika michuano hii na sasa wamewafikia Uruguay ambao nao ni Mabingwa mara 15.

FT’ 🇦🇷 Argentina 1 – 0 Brasil 🇧🇷
Di Maria 22′

Hatimae Lionel Messi anashinda Kombe lake la kwanza na Timu ya Taifa baada ya Argentina kuifunga Brazil leo goli 1-0 lililofungwa na Di Maria dakika 22 katika michuano ya Copa America.

Messi amefanikiwa kucheza fainali nne za Copa America 2007, 2015 na 2016 zote Argentina alipoteza kabla ya fainali ya nne leo kuandika historia mpya.

Messi amefanikiwa pia kuibuka mchezaji bora wa mashindano, mfungaji bora akiwa na magoli 4 na assist 5, amechangia katika magoli 9 ya Argentina kati ya 12 yaliofungwa katika michuano hii huku akicheza dakika zote 630 za michuano hiyo sawa na mechi 7.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tetesi za Soka Ulaya leo Alhamisi Septemba 23, 2021

Mshambuliaji wa Arsenal na Ufaransa Alexandre Lacazette, 30, hana hamu ya kusaini kandarasi mpya klabuni hapo. Mkataba wake wa

Read More...

Wanaharakati wa haki za binadamu wahoji hukumu dhidi ya Rusesabagina

 Makundi ya kutetea haki za binadamu barani Afrika yamelalamikia uamuzi wa mahakama kuu ya Rwanda ya kumfunga jela kwa miaka 25, Paul Rusesabagina ambaye alisifika sana kwenye filamu ya Hollywood ya Hotel Rwanda.  Mahakama hiyo Jumatatu ilisema kwamba imepata Rusesabagina pamoja na washukiwa wengine 20 na hatia ya

Read More...

LISSU NA WENZAKE WAFUTIWA KESI

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeifutia kesi ya uchochezi iliyokuwa inamkabili Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleao

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu