Arsenal amtaka kiungo wa Sevilla

In Kimataifa, Michezo

Imeelezwa kuwa mabosi wa Klabu ya Arsenal wanahitaji saini
ya nyota wa Klabu ya Sevilla, Joan Jordan ili kuongeza nguvu
ndani ya kikosi hicho.


Jicho la Kocha Mkuu wa Arsenal, Mikel Arteta linatajwa
kuitazama kwa ukaribu saini ya nyota huyo mwenye miaka 26
raia wa Hispania.

Ushindi wao wa mabao 3-1 dhidi ya Chelsea kwenye London
Dabi walioupata Desemba 26 umemfanya Arteta afikirie
kuongeza nguvu eneo la kiungo ili kupata ushindi zaidi kwenye
mechi zake.


Arteta ana matumaini kwamba akipata saini ya nyota huyo
ataongeza nguvu ya kujiamini kwa kikosi chake kwa kuwa ana
uwezo pia wa kufunga kwa kuwa ndani ya La Liga akiwa
amecheza jumla ya mechi 41 amefunga mabao mawili.


Arsenal ipo tayari kuweka dau la pauni milioni 32 ili kumpata
nyota huyo ambaye amewahi kucheza pia ndani ya Klabu ya
Eibar msimu wa 2017-19 na alicheza jumla ya mechi 71 na
kufunga mabao 10.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

RAIS MAGUFULI AZINDUA SHAMBA LA MITI SILAYO

Rais Dk John Magufuli leo amezindua na kubadilisha jina Shamba la Miti Chato na kuliita Shamba la Miti

Read More...

Kenya kutumia Teknolojia ya Roboti kudhibiti Corona.

Wizara ya Afya nchini Kenya imezindua Teknolojia ya kutumia Roboti ili kupambana na janga la virusi vya Corona na

Read More...

Rais wa Ethiopia atua Chato kwa ziara ya siku moja.

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la watu wa Ethiopia Sahle Work Zewde,amewasili nchini Tanzania tayari kufanya ziara

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu