The Gunners wamekubali kulipa dau la £1.8m kumsajili Odegaard lakini hawatakuwa na fursa ya kifungu cha kumnunua katika kandarasi hiyo (Times – subscription required)
Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer atamruhusu mshambuliaji wa England Jesse Lingard, 28, kuondoka kwa mkopo wakati wa dirisha la uhamisho la mwezi Januari lakini uamuzi wa mwisho utafanywa na bodi ya klabu hiyo ya Old Trafford . (ESPN)
Real Madrid huenda wakawa na hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Norway na Borussia Dortmund ,20, Erling Braut Haaland, ambaye anatakiwa na Chelsea na Man United baada mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, kusema kwamba anafurahia kualia Paris St-Germain. (Express)
