Arusha yatiliana sahihi na Kampuni ya Planet  Pharma ceutical  Ltd.

In Kitaifa

Serikali ya mkoa wa Arusha Leo, imetiliana sahihi na Kampuni ya Planet  Pharma ceutical  Ltd, ya mkoa Dar es salaam kwa ajili ya kutoa huduma za vifaa tiba na madawa kama muungozo wa wizara ya Afya maendeleo ya jamii wazee na watoto ilivyotoa.

Akitiliana sahihi na kampuni hiyo Katibu tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega amesema kuwa hii ni hatua kubwa kwa mkoa wa Arusha, kwa kuwa  hakutakuwa  na upungufu wa dawa baada ya kumpata kampuni hiyo.

Amesema kuwa mkataba huo umeambatanisha pamoja na bei utaenda hadi kwenye hospitali zote za  mkoani hapa, pamoja  na vituo vya Afya na zahanati kwa kuweza kuagiza moja kwa moja dawa na vifaa vyote vya matibabu kutoka kampuni hiyo.

Kwa Upande wake Afisa Manunuzi na Ugavi Mkuu mkoani hapa Elirehema Masanja amesema kuwa mchakato huo ulianzia mwezi mei mwaka huu, na wamepata  kampuni ya Planet Pharma ceutical yanye makao makuu jijini Dar es salaam, kwa ajili ya kutoa huduma za vifaa tiba na dawa kwa hospitali za serikali vituo vya Afya na zahanati zote mkoani hapa.

Amesema kuwa kampuni hiyo imeweza kushinda zabuni hiyo na itatakiwa kuanza mara moja kazi hiyo baada ya utiliaji saini huo, ikiwemo kutoa huduma za usambazaji wa vifaa tiba na madawa yanaokosekana kwenye vyetu vya Afya hapa mkoani mwetu.

Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Venu Madhav amesema kuwa kampuni hiyo ina uzoefu mkubwa wa kazi hiyo ambapo imekuwa ikifanyakazi hizo kwenye mikoa ya Dar es salaam, Mwanza na Shinyanga na sasa wamekuja Arusha na
wamejipanga kutoa huduma yenye tija kwa hospitali zetu mkoani hapa.

Amesema kuwa wamejipanga vizuri kuhakikisha wanatoa hudma bora na vifaatiba vyeny ubora unaokubalika kwani kampuni hiyo inauzoefu wa muda mrafu katika masuala hayo hapa nchini na nje ya nchi.

 

 

 

 

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu