Baada ya kupata mtoto wa tatu, Messi apewa zawadi ya kipekee na FC Barcelona

In Kimataifa, Michezo

Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi jana Machi 10, 2018 amepata mtoto wa tatu wa kiume aliyebatizwa kwa jina la Ciro.

Messi na familia yake wakiwa na Ciro

Kufuatia ushindi huo klabu ya Barcelona ambayo usiku wa kuamkia leo imepata ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Malaga, Kocha wa klabu hiyo, Ernesto Valverde amesema kuwa zawadi pekee ya Messi ni ushindi huo waliyoupata jana usiku kwani hakuna zawadi ambayo ingekamilisha furaha ya mchezaji huyo.

Nimeongea na Messi baada ya mchezo kumalizika, amesema anajiona mtu mwenye furaha zaidi kwa siku ya leo kwani mbali ya kupata mtoto lakini amefurahishwa zaidi na matokeo. Napenda kusema kuwa ushindi huu ni zawadi yake, hakuna zawadi nyingine kubwa kwa mchezaji wa Barcelona zaidi ya ushindi,“amesema Ernesto Valverde.

Mabao ya Barcelona yamefungwa na Luis Suarez dakika ya 15, na Philippe Coutinho, dakika ya 28 na kuifanya klabu hiyo kujikita kileleni kwa alama 72.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Jaji Mutungi avitahadharisha vyama vya siasa.

Vyama vya siasa nchini vimetakiwa kutekeleza majukumu yao ya kisiasa kwa kufuata na kuzingatia sheria na kanuni za vyama

Read More...

Bangi sasa ruksa Canada.

Canada imepitisha sheria rasmi kwa nchi nzima inayoruhusu matumizi ya bangi hadharani tofauti na hapo awali ambapo iliwabidi wananchi

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu