Barack Obama awataka Wamarekani kuwapinga vikali Viongozi wanaochochea ubaguzi.

In Kimataifa

Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama amewataka Wamarekani kukataa lugha za chuki na kibaguzi kutoka kwa viongozi wao.

 Obama amekuwa akiongea kwa nadra tangu alipoondoka madarakani, na japo hakumtaja kiongozi yeyote kwa jina, lakini kauli yake hiyo imekuja baada ya rais Donald Trump akiwa katika harakati za kujinasua kuwa kauli zake dhidi ya wahamiaji ndizo chanzo cha kuchochea mauaji nchini humo.

Katika hotuba yake jana Jumatatu, Trump alikemea ubaguzi wa rangi.

Jumla ya watu 31 wameuawa katika mashambulio ya bubduki kwenye majimbo ya Texas na Ohio mwishoni mwa wiki.

Akiwa madarakani, Obama alipambana bila mafanikio kudhibiti umiliki wa silaha za moto nchini Marekani. Alikiambia chombo kimoja cha habari mwaka 2015 kuwa, kushindwa kupitishwa kwa sheria za kudhibiti silaha ndilo jambo kubwa alilofeli akiwa kama kiongozi wa nchi hiyo.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

SOKA LA KIMATAIFA NA FUNUNU ZAKE

Real Madrid bado wanataka kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Brazili Neymar, lakini wanataka hakikisho kutoka Paris St-Germain kuhusu hali

Read More...

(TAMISEMI) KUTOA TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA.

Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani S Jafo kesho tarehe 23 Mwezi

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu