Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) limewataka Waislamu kujiepusha na mtu anayejiita mtume

In Kitaifa

Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) limewataka Waislamu kujiepusha na mtu anayejiita mtume na kufundisha mambo yanayopingana na Imani ya Kiislamu, eneo la Kibaha Misugusugu mkoani Pwani.

Akizungumza kwa niaba ya Mufti Shehe Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir jijini Dar es Salaam jana, Msemaji wa Mufti, Shehe Khamis Mataka  amesema Hamza Issa ndiye anayedai kushukiwa na roho ya Nabii Illyasa na kuwaaminisha watu kwenye mafundisho yake kuwa yeye ndiye Nabii Ilyasa.

Amesema baada ya kupokea maazimio ya Baraza la Mashehe wa Mkoa wa Pwani kuhusu taarifa za Hamza Issa kujiita mtume, Mufti Zubeir alikaa na Baraza lake la Ulamaa na kupitisha maazimio mbalimbali ikiwemo kuwaonya Waislamu, kuwa yeyote atakayemfuata Hamza Issa, atakuwa ametoka ndani ya Uislamu.

Shehe Mataka alitaja maazimio mengine yaliyopitishwa na Baraza la Ulamaa ni pamoja na kuwataka mashehe wa mikoa, wilaya na Maimamu, kutompa nafasi Hamza Issa ya kuzungumza misikitini wala kusikiliza CD zake ,ili kutoruhusu upotoshaji wake kuenea katika jamii.

Msemaji huyo wa Mufti alieleza kuwa Baraza la Ulamaa ni chombo cha kuchunga nidhamu ya dini katika Uislamu na kuongeza kuwa mafundisho yanayotolewa na Hamza Issa, kuhusu kuingiwa na roho ilyomfanya kuwa mtume ni mara ya kwanza kusikika duniani kwa mujibu wa Imani ya Kiislamu.

 

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu