Basi la abiria lakamatwa likiwa na abiria 95

In Kitaifa
Na Renalda Massawe
Katika operesheni ya ukaguzi wa magari ambayo imeanza jijini Arusha  leo July10 majira ya saa 06:00hrs asubuhi Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Arusha Mrakibu wa Polisi (SP)Joseph Bukombe akiwaongoza Askari katika barabara ya Arusha – Kiteto walifanikiwa kukamata Basi lenye Namba za Usajili T. 735 AEM mali ya Kampuni ya COAST LINE likiwa limepakia abiria 95.
Basi hilo ambalo linafanya safari zake kati ya Arusha na Kiteto lilikua limepakia abiria 67 ambao walikua wamekaa kwenye siti, 25 walikua wamesimama,  kati yao Abiria wa kawaida walikua 10  na Wanajeshi 15. Pamoja na hao walikuepo Dereva, kondakta, fundi na Msindikizaji wa basi hilo ambapo wanafanya  idadi yao kuwa 95.
Akizungumza na  Abiria wa Basi hilo Mkuu huyo wa Usalama Barabarani (RTO)Josephy Bukombe amewataka kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi pindi wanapoona Basi limezidisha abiria, mwendo mkali na kutokubali kupanda basi ambalo limejaa.
Aidha ametoa wito kwa wamiliki wa Mabasi kuwasimamia Wafanyakazi wao hasa madereva na Makondakta ili waweze kufuata sheria bila kushurutishwa.
Meneja wa Mabasi ya Coast Line Bwana Petro Amsi Stanley amepongeza Operesheni hiyo inayoendelea kufanywa kwani itasaidia kuwadhibiti Madereva na Makondakta wanaofanya kazi bila kufuata sheria  kwa sababu Wamiliki na Mawakala wanakua hawana taarifa za abiria kuzidi kwenye mabasi yao.
Pia amempongeza Mkuu wa Kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Arusha kwa kazi nzuri anayoendelea kuifanya kwa ufasaha.
Basi hilo limefikishwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kufanyiwa  Ukaguzi zaidi.
Aidha Mkuu wa  wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Arusha ameamuru wakala wa basi hilo awatafutie abiria  wote waliozidi usafiri mwingine.
Sambamba na hilo, Dereva na Kondakta wa basi hilo wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano, mara baada ya Upelelezi kukamilika watafikishwa Mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

SOKA LA KIMATAIFA NA FUNUNU ZAKE

Real Madrid bado wanataka kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Brazili Neymar, lakini wanataka hakikisho kutoka Paris St-Germain kuhusu hali

Read More...

(TAMISEMI) KUTOA TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA.

Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani S Jafo kesho tarehe 23 Mwezi

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu