Baunsa Anayedaiwa Kumuua Mowzey Radio Atiwa Mbaroni.

In Kitaifa
Mtuhumiwa namba moja ambaye anayedaiwa kuhusika na kifo cha msanii muziki nchini Uganda, Mowzey Radio amekamtwa na Jeshi la Polisi nchini humo.

Kijana Wamala Godfrey mwenye umri wa miaka 28 ndiye alikuwa akisakwa na jeshi la polisi kama mtuhumiwa mkuu mara baada ya mmiliki wa bar, Egesa George na Meneja wake kilipotokea kifo cha Radio kushikiliwa na Polisi.
Wamala alikamatwa katika eneo la Kyengera alipokuwa amejificha kwa siku kadhaa nyumbani kwa rafiki yake. Wamala amehamishiwa mjini Entebbe.
Mwimbaji Mowzey Radio alifariki dunia Februari Mosi mwaka huu kutokana na majeraha ambayo aliyapata kichwani kufuatia ugomvi katika bar hiyo.
Kamanda wa Polisi Kampala, CP. Frank Mwesigwa amethibitisha kushikiliwa kwa Wamala Godfrey na kueleza kuwa kwa sasa wanaandaa majalada ili kuweza kumfikisha mahakamani.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu