Biden anatarajiwa kufanya uteuzi wa kwanza wa mawaziri wiki hii

In Kimataifa

Rais mteule wa Marekani Joe Biden atafanya uteuzi wa kwanza wa baraza la mawaziri Jumanne wiki hii, kulingana na taarifa iliyotolewa na mkuu wake wa utumishi. Rais Donald Trump ameendelea na madai yake ya kuwepo na udanganyifu katika uchaguzi wa rais na kuongezeka kwa upinzani ndani ya chama chake mwenyewe huku akikataa kukubali kushindwa. Biden ameendelea na maandalizi ya kuchukua madaraka ifikapo Januari 20, licha ya jaribio la Trump la kutaka kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa Novemba 3. Trump amepata pigo jingine baada ya kesi yake ya kupinga matokeo kutupiliwa mbali. Hii ni baada ya timu ya kampeni ya Trump kuwasilisha kesi mahakamani iliyonuia kupinga matokeo ya kura zilizopigwa kwa njia ya posta katika jimbo la Pennsylvania.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

RAIS MAGUFULI AZINDUA SHAMBA LA MITI SILAYO

Rais Dk John Magufuli leo amezindua na kubadilisha jina Shamba la Miti Chato na kuliita Shamba la Miti

Read More...

Kenya kutumia Teknolojia ya Roboti kudhibiti Corona.

Wizara ya Afya nchini Kenya imezindua Teknolojia ya kutumia Roboti ili kupambana na janga la virusi vya Corona na

Read More...

Rais wa Ethiopia atua Chato kwa ziara ya siku moja.

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la watu wa Ethiopia Sahle Work Zewde,amewasili nchini Tanzania tayari kufanya ziara

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu