Bobi Wine akamatwa tena baada ya kuzuiwa kuondoka Uganda.

In Kimataifa

Mbunge wa Upinzani nchini Uganda ambaye pia ni mwanamuziki Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine ambaye anadaiwa kupigwa na kuteswa baada ya kukamatwa mapema mwezi huu, inasemekana amezuiwa kuondoka kwa ajili ya kwenda kupata matibabu nje ya nchi.

Akizungumzia kukamatwa kwa mteja wake, Mwanasheria wa Mbunge huyo Robert Amsterdam amesema Bobi Wine alizuiliwa kuingia katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Uganda na kuchukuliwa na polisi ambao wanadaiwa kumpeleka katika hospital ya serikali.

”..licha ya kwamba Jaji alitaka apewe pasi yake ya kusafiria kwa sababu anahitaji kuondoka nchini humo kwa sababu ya kwenda kupata matibabu nje, kufuatia mateso makali ambapo yeye na wabunge wengine 33 wa upinzani waliyapata, amechukuliwa kikatili na gari la wagonjwa la polisi, Mawakili hawajui wapi alipopelekwa na tumepatwa na mshtuko..” Alisema wakili wa Bobi Wine

Kabla ya Kuzuiliwa kwa Bobi Wine, mbunge mwingine tena wa upinzani Francis Zake pia alizuia Uwanja wa ndege kwa ajili ya kwenda kupata matibabu nje ya nchi.

Bobi Wine anakabiliwa na makosa ya uhaini, kufuatia tukio la kushambuliwa kwa mawe gari la Rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni. Aliachiliwa kwa dhamana kutoka kizuizini alikokuwa akishikiliwa siku ya Jumatatu, akiwa katika hali mbaya.

Mwanasheria wake Robert Amsterdam anasema kipaumbele cha Bobi Wine ni kupata matibabu na si kuitoroka nchi.

”…Watoto wake watabaki nchini Uganda, ni safari ya muda mfupi, kwa ajili tu ya kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu. Anakabiliwa na maumivu makali… alifafanua

Amesema anamajeraha makubwa yaliyosababishwa na kuteswa kwake na vitu vya chuma na vifaa vingine vilivyotumika kumtesea na anahitaji msaada.

”.. Tuseme kuwa hakuna kiungo chake chochote cha mwili kisichouma na na ana matatizo makubwa katika figo lake…” aliongeza wakili wake

Siku ya Jumatano Spika wa Bunge la Uganda alitaka kukamatwa kwa maafisa usalama walioshiriki kumpiga mbunge huyo.

Hata hivyo serikali ya Uganda imekataa madai kuwa Bobi Wine alitendewa vibaya wakati alipokuwa kizuizini.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

CAF YAWAPIGA CHINI MAREFA WA TANZANIA AFCON 2019, YACHUKUA HADI WA BURUNDI,KENYA,TANZANIA HOLAA.

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya marefa 27 na marefa wasaidizi 29 kwa ajili ya Fainali za

Read More...

Man U, Juventus wafungishwa virago UEFA

Timu ya Manchester United imeondoshwa katika michuano ya ligi ya mabingwa ulaya hatua ya robo fainali baada ya kukubali

Read More...

Arsenal yarejea nafasi ya nne ligi kuu.

Arsenal yafanikiwa kurejea tena nafasi ya nne katika jedwali la ligi ya premia baada ya ushindi wake dhidi ya

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu