Bobi Wine atiwa mbaroni Uganda

In Kimataifa

Mwanasiasa wa Uganda ambaye pia alikuwa mgombea urais wa Chama cha Upinzani, Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine, amekamatwa katika mji Mkuu wa Kampala.

Taarifa zinasema wakati Bobi Wine anakamatwa, alikuwa anaongoza timu ya wabunge kutoka Chama chake cha National Unity Platform, kufanya maandamano dhidi ya kukamatwa na kutoweka kwa wafuasi wa chama chake katika kipindi cha kuelekea, wakati na baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika Januari.

Vikosi vya usalama vilifyatua vitoza machozi na kutawanya waandamaji waliokuwa wameandamana na mwanasiasa huyo.

Inasemekana kwamba waliokamatwa ni pamoja na wabunge 15.

Katika mkutano uliofanyika kupitia njia ya video, Bobi Wine alitoa wito kwa wafuasi wake kutumia njia za amani kuandamana dhidi ya matokeo ya uchaguzi – ambayo anaendelea kudai kuwa vikosi vya usalama itoe wale wasiojulikana walipo

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu