BODI NA MABARAZA YA KITAALUMA JIPANGENI KURUDISHA ASILIMIA YA FEDHA KWENYE MIKOA: DKT. GWAJIMA

In Kitaifa

Bodi na Mabaraza yote ya kitaaluma ya sekta ya afya yametakiwa kujipanga kurejesha asilimia ya fedha wanazokusanya kwenye Mikoa na Halmashauri ili wasajili wasaidizi wawajibike katika ngazi za mikoa na halmashauri na kuharakisha kuwahudumia wananchi.

Hayo yamesemwa leo na Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati wa Uzinduzi wa Bodi Mpya ya Bodi ya Ushauri wa Hospitali Binafsi iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma. “Hivyo mganga Mkuu wa serikali unayesimamia Mabaraza na Bodi hizi simamia hii mara moja mlete mapendekezo nini tufanye ili litokee”.

Kwa upande mwingine, Dkt. Gwajima amesema kuwa uzinduzi wa bodi mpya ya ushauri wa hospitali binafsi ni tukio muhimu linaloashiria utekelezaji wa ilani ya uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020-2025 kwa upande wa sekta ya afya kuwa, Serikali itaimarisha na kuhakikisha jamii inapata huduma za afya zilizo bora na salama kwa ushirikiano na Sekta binafsi. “Wajibu wenu kama bodi ni kuhakikisha kuwa mnasimamia na kudhibiti Hospitali Binafsi ambazo zinasimamiwa na watu au mashirika yaliyoidhinishwa pamoja na utendaji wao ili kuhakikisha jamii inapata huduma za Afya bora nchini.

Hivyo Bodi inawajibu wa kuhakikisha kuwa wamiliki na watumishi wa hospitali mnazozisimamia wanaelewa sheria, kanuni, taratibu na miongozo waliyosajiliwa ili ziendelee kutoa huduma kwa kufuata miiko na maadili”. amesisitiza Dkt. Gwajima

Hata hivyo ameitaka bodi hiyo kuhakikisha kuwa inakumbukumbu na taarifa sahihi za hospitali na mashirika binafsi inazozisajili/idhinisha na ambazo zinaweza kupatikana kiurahisi ili kuhakikisha jamii inapata taarifa sahihi ya Hospitali zilizosajiliwa au Mashirika yaliyoidhinishwa kutoa huduma pamoja na kutangaza majina ya Hospitali na Mashirika hayo walau mara moja kila mwaka kwenye gazeti la Serikali.

Dkt. Gwajima ameahidi kushirikiana na kuwawezesha bodi hiyo wakati wote wanapohitaji msaada ili kazi zao ziwe nyepesi na zenye matokeo ya haraka kwa wananchi na kuwaasa kujiepusha na mambo yasiyo kuwa na uadilifu katika kutekeleza kazi hiyo kwa kuwa wameaminiwa.

Naye Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya ushauri wa hospitali binafsi ambaye pia ni Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Aifelo Sichalwe amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita inatambua mchango wa sekta binafsi hivyo serikali itaendelea kutoa mashirikiano kwenye eneo hilo pamoja nay ale ya nchi nyingine .

Amesema Serikali itaendelea kutoa miongozo na kuhakikisha sekta binafsi inatekelezeka hivyo bodi hiyo itasaidia kutatua changamoto kwani wanatambua faida ya ubia na kujifunza kutokana na mashirikiano hayo.

Wakati huo huo Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Bi. Ziada Sella amewataka wajumbe wapya kupitia sheria, kanuni na miongozo kwa kushirikiana na viongozi wa Bodi waliopita ili kuweza kuwa na nafasi nzuri ya kushughulikia utekelezaji wa shughuli za bodi na maagizo yaliyotolewa na Waziri wa Afya.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu