Bosi wa CIA kuhojiwa na bunge la Seneti Marekani, Mauaji ya Khashoggi.

In Kimataifa

Mkurugenzi wa shirika la ujasusi la Marekani Bi Gina Haspel atafanya mahojiano na wajumbe wa bunge la Congress juu ya mauaji ya mwanahabari Jamal Khashoggi.

Vyombo vya habari nchini Marekani vinaripoti kuwa bi Haaspel atakutana na viongozi wa bunge la Seneti baadae leo Jumanne.

Mkurugenzi huyo hakuwepo wiki iliyopita wakati mawaziri wa mambo ya nje na ulinzi walipofanya mazungumzo na viongozi wa Seneti, kitendo ambacho kiliwakasirisha baadhi ya wajumbe wa bunge hilo.

Khashoggi aliuawa ndani ya ofisi za ubalozi mdogo wa Saudi Arabia jijini Istanbul, Uturuki Oktoba 2. Mwanahabari huyo alikuwa ni mkosoaji mkubwa wa sera za Saudia hususani mwanamfalme Mohammed bin Salman.

Vyombo vya habari vya Marekani pia vimeripoti kuwa ripoti ya CIA juu ya mkasa huo inaonesha kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa bin Salman aliamuru mauaji hayo.

Tayari Saudia imewashitaki watu 11 juu ya mauaji hayo, lakini wanakanusha vikali juu ya uhusika wa bin Salman.

Vyombo vya habari nchini Marekani pia vinaripoti kuwa CIA wana ushahidi unaonesha kuwa bin Salman aliwasiliana kwa wa ujumbe nfupi wa simu ya mkononi na Saud al-Qahtani ambaye inadaiwa ndiye aliyeendesha operesheni ya mauaji ya Khashoggi.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Kitambulisho cha Vladimir Putin cha ujasusi chapatikana Ujerumani.

Kitambulisho cha Vladimir Putin alichopewa kama jasusi Ujerumani alipokuwa anafanya kazi kama jasusi wa Urusi kimepatikana katika makavazi mjini

Read More...

May aairisha kura kuhusu Brexit.

Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May ameahirisha kura iliyokuwa ifanyike leo bungeni kuhusu makubaliano ambayo serikali yake na Umoja

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu