BOT AZITAKA TAASISI ZA KIFEDHA KUZINGATIA UADILIFU

In Kitaifa
Naibu Gavana wa benki kuu Tanzania (BOT) Dr.Bernard Kibesse  amezitaka taasisi za kifedha kuzingatia uwadilifu katika utoaji wa huduma za kifedha hasa katika zama hizi za kidigitali ili kuwahahikishia wateja wao usalama wa fedha zao.
Akizungumza katika  kongamano LA
 Taasisi za kifedha za Afrika Mashariki linaloendelea jijini Arusha ,Naibu Gavana amesema kuwa licha ya changamoto za wizi kwa njia za mitandao bado taasisi hizo zina jukumu la kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu Mkubwa kwani ndio nguzo kuu ya huduma hizo.
Aidha amesema kuwa serikali haitasita kuwachukulia hatua taasisi za kifedha zinazokiuka sheria ,maadali na tararibu za utoaji wa huduma ikiwemo kuzinyang’anya leseni .
Patrick mwisusa ni  mkurugenzi mtendaji wa  Tanzania institute of bankers amesema kuwa kongamano hilo linalenga kuangalia maswala ya nafasi ya maadili katika utoaji wa huduma za kifedha na kuhimiza suala la uadilifu katika kulinda tasnia ya fedha Katika nchi za Afrika Mashariki
Mshiriki wa kongamano  ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi za Kifedha nchini Kenya  Kenya,  Gilbert Allela amesema kuwa taasisi za fedha zina nafasi Mkubwa ya kulinda na kutunza uaminifu wa wateja wao kwa kujifunza mbinu za kisasa za kukabiliana na wizi wa kimtandao.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MAJANGILI SUGU WAKAMATWA ARUSHA.

Jeshi la polisi mkoani Arusha kushirikiana na kikosi kazi kinachojihusisha na TANAPA, mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro, kikosi dhidi

Read More...

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, na wa Uganda waweka mikakati ya kushirikiana.

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Felix Tshisekedi amekuwa katika ziara ya siku mbili nchini Uganda kwa ajili

Read More...

Wagombea walioenguliwa waruhusiwa kushiriki Uchaguzi

Waziri wa Nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo ametangaza kuwaruhusu wagombea wote waliochukuwa fomu na kuzirejesha kwa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu