CAG na Mdee kuhojiwa kwa kulidhalilisha Bunge.

In Kitaifa

Spika wa Bunge Job Ndugai amemtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Profesa Mussa Assad kufika mbele ya Kamati ya Maadili ya Bunge Januari 21, 2019 kwa hiari kwa ajili ya kuhojiwa, vinginevyo atapelekwa kwa pingu.

Mbali na CAG mbunge wa Kawe Chadema Halima Mdee, naye ameitwa mbele ya kamati hiyo siku inayofuata yaani Januari 22 2019.

Spika Ndugai ametoa kauli hiyo leo mchana alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, akisema Profesa Assad amelidhalilisha Bunge.

Ndugai amesema CAG akiwa nje ya Tanzania wakati anahojiwa na Idhaa ya Kiswahili, alisema Bunge la Tanzania kuwa ni dhaifu.

Kama kilikupita alichokisema CAG basi tunakusogezea hapa umsikie sababu ya kutakiwa kuhojiwa na bunge.

Baada ya kauli hiyo ya Profesa Assad wiki iliyopita Halima Mdee alihojiwa na baadhi ya vyombo vya habari kuhusu alichokisema CAG na kukubaliana na hoja zake.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Majeshi ya Marekani yauwa raia Somalia

Majeshi ya Marekani yanayoendesha mashambulizi ya angani nchini Somalia dhidi ya ngome za wapiganaji wa Al Shabab nchini humo

Read More...

Idai yapoteza makazi ya watu 400,000.

Shirika la Msalaba Mwekundu linakadiria kuwa watu 400,000 wamepoteza makaazi yao nchini Msumbiji kutokana na Kimbunga Idai kilichoipiga nchi

Read More...

Baa la njaa kuikumba Kenya.

Zaidi ya watu milioni 1.5 nchini Kenya wako katika hatari ya kukabiliwa na baa la njaa kufuatia kutokuwepo kwa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu