Cairo jiji hatari zaidi kwa wanawake duniani.

In Kimataifa

Jiji la Cairo ndilo hatari zaidi kwa wanawake kuishi duniani miongoni mwa majiji duniani, utafiti wa shirika la Thomson Reuters Foundation unaonesha.
London nao ndio mji bora zaidi kwa wanawake kuishi.
Mji wa Kishasha nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo unafuata Cairo, nao mji wa Lagos nchini Nigeria ni wa nane kwenye orodha hiyo.
Jumla ya majiji 19 makubwa yalichunguzwa – ambayo ni majiji yenye idadi ya watu inayofika milioni kumi na zaidi.
Miongoni mwa yaliyozingatiwa kwenye utafiti huo ni unyanyasaji wa kingono, utamaduni unaowadhalilisha wanawake pamoja na upatikanaji wa huduma bora ya afya kwa wanawake, fedha na elimu.
Wataalamu katika haki za wanawake waliombwa ushauri wao wakati wa kufanywa kwa utafiti hao, miongoni mwao akiwa mwanahabari Shahira Amin, ambaye aliambia Thomson Reuters:
“Mambo yote kuhusu wanawake katika jiji hilo ni hatari. Hata kutembea tu barabarani, na hunyanyaswa sana, kwa maneno na kwa vitendo.”

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu