CARDI B AWAJIBU WANAOMUITA MKANDAMIZAJI NA MBAKAJI.

In Burudani

Msanii wa kike wa HipHop kutokea nchini Marekani Cardi B, amewajibu watu wote ambao wanamuita mkandamizaji na mbakaji, kwa kitendo chake cha kuwaibia wanaume pesa kabla hajatoka kimuziki.

Cardi B amefunguka hayo kupitia “Insta Live” ya mtandao wa kijamii wa Instagram baada ya watu wengi kumtukana na kumkashifu kwa kitendo hicho na kumuita mkandamizaji na mbakaji . “Sipendi kusikia watu wakijaribu kuniita mkandamizaji au mbakaji, sipendii hii kitu kwa sababu watu wanapenda kutafuta vitu ambavyo vingine sijavifanya, sijamgusa mwanaume yeyote na sijafanya na mwanaume yeyote, na suala la kubaka ni kufanya kwa kutumia nguvu bila idhini ya mtu na bila kuuliza, huu ni uongo na sijafanya vitendo hivyo”. Aidha msanii huyo amekubali kitendo cha kuwaibia wanaume pesa zao kwa kutumia njia ya kuwaekea madawa kwenye vinywaji na kisha kuwaiba pesa zao, kipindi alipokuwa mnenguaji maarufu wa klabu zililzopo jijini New York City, kabla ya kuwa msanii wa muziki.

Ikumbukwe tu mapema mwezi wa tatu mwaka huu Cardi B, alitangaza kuwa aliwahi kuwa mnenguaji maarufu kwenye klabu, na pia alikua anatumia wanaume ili kupata pesa kwa kuwaekea madawa ya kulevya na kufanya nao mapenzi kisha kuwabia pesa zao.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

SOKA LA KIMATAIFA NA FUNUNU ZAKE

Real Madrid bado wanataka kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Brazili Neymar, lakini wanataka hakikisho kutoka Paris St-Germain kuhusu hali

Read More...

(TAMISEMI) KUTOA TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA.

Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani S Jafo kesho tarehe 23 Mwezi

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu