Chid Benz mbaroni tena!

In Burudani

Msanii mkongwe wa Bongo Fleva, Rashid Makwiro maarufu kama ‘Chid Benz’ amekamatwa na Jeshi la Polisi jijini Dodoma kwa tuhuma za kukutwa na mzigo wa bangi kiasi cha gramu 5.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amesema hayo leo Jumatatu, Juni 18, 2018 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini humo baada ya kumtia mbaroni msanii huyo.

Hii ni mara ya nne kwa Chidi Benz kukamatwa na madawa ya kulevya huku akidai kuwa alishaacha kutumia madawa hayo na anaendelea na matibabu Sober House.

Mnamo Disemba 30, 2017 nguli huyo wa Hip Hop Chid Benz alishikiliwa tena  na jeshi la polisi mkoani Dodoma akiwa na mke wake ambapo alikamatwa na dawa za kulevya aina ya Heroine na kufikishwa mahabusu.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Mwili Mwingine Waonekana Ukielea karibu na kivuko cha Mv Nyerere.

Mwili mmoja wa mtoto umepatikana saa nne asubuhi ya leo, wakati wazamiaji wakiweka sehemu ya chini Maputo (boya) yanayojazwa

Read More...

Okoth Obado: Gavana wa Migori afikishwa mahakamani Kenya katika kesi ya mauaji ya Sharon Otieno.

Mwansiasa mkuu nchini Kenya leo amefikishwa mahakamani katika mji mkuu Nairobi kwa mashtaka ya kusaidia na kupanga mauaji. Gavana

Read More...

Magazeti ya leo Septemba 24, 2018.

Magazetini leo Jumatatu September 24,2018

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu