China na Marekani kumaliza mgogoro wa kibiashara.

In Kimataifa

China imekubali kununua bidhaa na huduma za Marekani zaidi, kwa lengo la kupunguza mgogoro wa usawa wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili na hivyo kuondoa hofu ya kuibuka kwa vita ya kibiashara.

Washington wamesema, hatua hiyo itasaidia “kupunguza gharama” ambayo kwa mwaka kibiashara China hupata upungufu wa Dola bilioni 335.

Lakini hata hivyo taarifa hiyo haijaeleza zaidi kuhusu punguzo hilo kubwa litakavyokuwa.

“Pande zote mbili zimekubaliana kwa mantiki hiyo ya maana ya kuongeza uuzaji wa bidhaa za kilimo na nishati nchini Marekani ,” imesema sehemu ya taarifa ya pamoja kati ya Marekani na China baada ya mazungumzo ya siku kadhaa yaliyofanyika nchini Marekani.

“Hali hii itasaidia kukua na kuongeza ajira ndani ya Marekani.”
Nchi hizo pia zimekubaliana kuendelea kuyasimamia makubaliano ya biashara kwa lengo la kuondoa wasiwasi wao “kwa maana inayofaa”.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu