CUF watoa maazimio Mazito.

In Kitaifa, Siasa
MAAZIMIO YA KIKAO CHA KAWAIDA CHA KAMATI YA UTENDAJI YA TAIFA YA THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-CHAMA CHA WANANCHI) KILICHOFANYIKA TAREHE 25 MACHI, 2018-DAR ES SALAAM:
1. Kamati ya Utendaji ya Taifa ilikutana Tarehe 25 Machi katika Ukumbi wa Ofisi ya Wabunge wa CUF uliopo Magomeni, Dar es Salaam chini ya Uenyekiti wa Katibu Mkuu.
2.     Kikao kilijadili ajenda kadhaa, zikiwemo:
a)    Hujuma zinazopangwa na Profesa Ibrahim H. Lipumba na genge lake dhidi ya CUF.
b)    Maandalizi ya Uchaguzi wa Chama ndani ya Chama.
c) Taarifa ya Maendeleo ya kesi za CUF zilizoko Mahakamani.
d)    Hali ya kisiasa nchini.
Maamuzi ya Kamati ya Utendaji ya Taifa yalikuwa kama ifuatayo:-
  1.Kuhusu HUJUMA zinazopangwa na kutekelezwa na Lipumba na genge lake wakishirikiana na Msajili wa Vyama vya Sasa nchini:-
Kamati ya Utendaji ya Taifa ilipokea taarifa za kina za hujuma dhidi ya CUF na kuazimia ifuatayo:-
(i) Chama kiendelee kufuatilia hujuma hizo kwa lengo la kudhibiti.
(ii) Imewaagiza viongozi na wanachama wa ngapi zote kuwa makini na kufuatilia hila zote za kukihujumu Chama na kuwafichua wale wote watakaogundulikana kuwa na nia ya kukihujumu Chama.
(iii) Wanachama wasikubali kuchokozeka, lakini hapo hapo kuwadhibiti wale wote ambao wamekusudia na kufanya njama za kukivuruga Chama.
(iv)Wanachama waimarishe umoja,  mashirikiano na mshikamano, wakitambua kuwa umoja ni silaha mujarabu ya kuwashida maadui wa Chama.
(v)Wanachama wanatakiwa kumpuuza Lipumba, genge lake na propaganda zao za kijinga.
(vi)Wanachama wanatakiwa kuwatenga na kutowapa mashirikiano mtu yeyote atakayebainika ni muasi wa Chama anayemuunga mkono Lipumba na genge lake.
2. Kuhusu Maandalizi ya Uchaguzi ndani ya Chama, Kamati ya Utendaji ya 
   Taifa, imeamua ifuatavyo:
(i) Wanachama wanatanabahishwa kuwa Baraza Kuu Halali  la Uongozi la Taifa la CUF lililochaguliwa June, 2014 bado halijakaa na kutoa maagizo ya Maandalizi ya Uchaguzi wa Chama ndani ya Chama. Wala Baraza Kuu halijatoa agizo lolote kwa Kamati ya Utendaji ya Taifa kuanza jambo lolote linalohusu Maandalizi hayo.
(ii)  Viongozi wa CUF katika ngapi za Wilaya,  Majimbo, Kata na Matawi  pamoja na Wanachama wote kwa jumla wanatakiwa  kupuuza yote yaliyotangazwa na Lipumba juu ya Maandalizi ya Uchaguzi wa Chama ndani ya Chama.
  (iii) Wanachama wanaombwa kuwa wastahamilivu juu ya hili, na wakati utapofika wa Kamati ya Utendaji Halali ya Chama Taifa kufanya maamuzi juu Maandalizi ya Uchaguzi wa Chama ndani ya Chama taarifa rasmi itatolewa kwa viongozi wa ngazi zote na wanachama wa kawaida.
3. Kuhusu Taarifa ya Maendeleo ya kesi za Chama, Kamati ya Utendaji ya Taifa;
(i)Inawapongeza kwa dhati mawakili wanaokiwakilisha Chama katika kesi hizo kwa kuzisimamia kwa dhati na kwa weledi wa hali ya juu na kuwaomba waendelee na moyo huo huo wa kuyatetea kwa nguvu zao zote masilahi ya Chama chetu.
(ii) Inawapongeza kwa dhati Kaimu Naibu Katibu Mkuu (B), Mhe. Joran Bashange, kwa kujiltolea kwa hali na Mali kufuatilia kesi za chama kwa karibu na kuwapa mashirikiano ya hali ya juu mawakili wetu.
(iii)Inawaomba wanachama na wapenzi wa Chama hasa wanaoishi Dar es Salaam na viunga vyake waendelee kujitokeza kwa wingi mahakamani kila siku ambayo kesi zetu zimepangwa kusikilizwa.
4. Kuhusu Hali ya kisiasa nchini, Kamati ya Utendaji ya Taifa baada ya mjadala wa kina imeamua kuwa :
(i) Kuendelea kufuatilia kwa makini malalamiko ya baadhi ya wananchi juu ukiukwaji wa haki za binadamu na kisha kushauriana na wadau wote, ikiwemo Serikali , juu ya kubaini ukweli wa malalamiko hayo, kujua chanzo chake na kuweka mikakati ya kuikomesha hali hiyo.
(ii)Kuikumbusha Serikali kuwa jukumu lake la msingi ni kulinda usalama wa raia na Mali zao. Hivyo Jeshi la polisi na vyombo vyenginevyo vya ulinzi vijiimarishe kutimiza wajibu huo kwa weledi wa hali ya juu.
(iii)Kuwa kumbusha wananchi watimize wajibu wao wa kutetea haki na  kuhakikisha kuwa Tanzania inaendelea kuwa na amani kwa kutofumbia macho vitendo vyote viovu vinavyoweza kuitikisa msingi madhubuti ya Taifa letu, ikiwemo Umoja na Mshikamano. Kila mwananchi kutendewa haki bila ya kujali kabila lake, dini yake, itikadi yake ya kisiasa na wala mahala alipozaliwa.
Mwisho:
Kamati ya Utendaji ya Taifa inatoa wito kwa Watanzania wote kuwa kitu kimoja katika kutetea maslahi mapana ya nchi yetu na watu wake, na kuendelea na utamaduni wetu wa kuhurumiana na kushirikiana katika wakati wa majaribu na wakati wa furaha.
AHSANTENI.
HAKI SAWA KWA WOTE
Imetolewa na Kamati ya Utendaji ya Taifa;
SEIF SHAIRF HAMAD
KATIBU MKUU
26 Machi, 2018

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu