David Luiz kuitangaza Rwanda Kimataifa.

In Kimataifa, Michezo

Mchezaji wa klabu ya Arsenal, David Luiz ameahidi kuitangaza Rwanda kimataifa kwenye sekta ya utalii kwa marafiki zake wanaoishi Ulaya na nchini kwao Brazil.

Akiongea na waandishi wa habari wikiendi iliyopita Jijini Kigali nchini Rwanda, David Luiz amesema kuwa atajitahidi kuwashawishi marafiki zake waitembelee nchi hiyo wanapokuwa likizo. “Nimefurahi sana kuwa hapa Rwanda, Tangu siku ya kwanza nafika hapa. Nadhani siku za mbeleni nitarudi tena,“Ameeleza David Luiz na kujibu aliyojionea wakati alipotembelea mbugani. “Tulitembea sana msituni na nimefurahi sana kuwaona sokwe mtu, Nitaenda kuwambia pia rafiki zangu wanaoishi Ulaya na Brazil, kuitembelea Rwanda pindi wanapopata likizo,” – amesema David Luiz.

David Luiz alikuwa nchini Rwanda kwa siku mbili, Kwenye ziara yake ya kikazi kupitia mradi wa kutangaza utalii nchini humo wa Visit Rwanda ambao umesainiwa mwaka jana kati ya Serikali ya Rwanda na klabu hiyo.

Luiz akiwa nchini humo pia alitembelea makumbusho ya mauaji ya kimbari, Hifadhi ya mlima volcano, na kukaribishwa Ikulu na Rais kagame.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tetesi za soka Ulaya.

Inter Milan wanafikiria kumnunua kiungo wa kati, Mfaransa N'Golo Kante huku Blues wakiwa tayari kusikiliza ofa kwa ajili

Read More...

Manchester City kushiriki kombe la Ulaya.

Klabu ya Manchester imefanikiwa kubadili marufuku ya miaka miwili kushiriki katika mashindano ya klabu bingwa Ulaya kuanzia msimu

Read More...

Mama akiri kuua Watoto wake wanne.

Mwanamke mmoja nchini Kenya Betrice Mwende, anayeshikiliwa kwa tuhuma za kuwaua watoto wake wanne, amekiri Mahakamani kuwa ni

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu