Dk. Bashiru Awakaribisha CCM Wanawake Imara wa Upinzani.

In Kitaifa

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ali, amesema chama chake kinawakaribisha wanasiasa wanawake ‘shoka’ wa upinzani watakao hitaji kujiunga na chama hicho.
Dk. Bashiru aliyasema hayo jana jijini hapa, wakati alipokuwa akifungua semina ya siku mbili kwa sekretarieti ya CCM na kamati za utekelezaji za jumuiya tatu za chama hicho.

Alisema katika uchaguzi mkuu 2020, wanawake kutoka vyama vya upinzani pamoja na wa CCM, wameonyesha ushindani mkubwa wa kisiasa hali iliyoonyesha walivyo na uwezo mkubwa wa uongozi.

“Mwaka huu tumeona nguvu ya kinamama wa upinzani na hata ndani ya CCM, katika kupambana kwenye nafasi za ubunge haijalishi wapo katika chama kikubwa au kidogo cha siasa kutokana na hali hii napenda kuwaambia kinamama wa vyama vya upinzani majembe wenye uwezo karibuni CCM,” alisema Dk. Bashiru.

Kadhalika, alisema kutokana na wanasiasa wanawake kuwagaragaza wagombea wa ubunge wanaume katika uchaguzi mkuu 2020, inamaanisha kuwa wana uwezo mkubwa ambao chama kinatakiwa kuutumia.

“Kama yule mbunge mwanamama wa CHADEMA aliyemshinda Kessy (Ally) kule Jimbo la Nkasi Kaskazini, pale kumtoa Kessy siyo jambo jepesi inatakiwa mtu mwenye uwezo, lakini pale Mbeya Mjini kwa Naibu Spika, hali hii inamaanisha kuwa kinamama wanastahili kupelekwa kwenye majimbo magumu ili kuyarejesha,” alisema Dk. Bashiru.

Aliziagiza jumuiya za CCM kufanya uchunguzi na tathmini ya kina kubaini mamluki na maadui waliokihujumu chama wakati wa uchaguzi mkuu, Oktoba 28, mwaka huu.

Dk. Bashiru alisema uchaguzi huo umeweka historia ya aina yake katika demokrasia za vyama vingi nchini ambao umeonyesha dhahiri maadui wa nchi na marafiki wa kweli kupitia mijadala na hoja mbalimbali zilizoibuka.

Alisema ushindi uliopatikana ni matokeo ya uchapakazi wa jumuiya zote kupitia mabalozi wa CCM zaidi ya 250,000 ambao ndio wenyeviti wa mashina ya chama.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

RAIS MAGUFULI AZINDUA SHAMBA LA MITI SILAYO

Rais Dk John Magufuli leo amezindua na kubadilisha jina Shamba la Miti Chato na kuliita Shamba la Miti

Read More...

Kenya kutumia Teknolojia ya Roboti kudhibiti Corona.

Wizara ya Afya nchini Kenya imezindua Teknolojia ya kutumia Roboti ili kupambana na janga la virusi vya Corona na

Read More...

Rais wa Ethiopia atua Chato kwa ziara ya siku moja.

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la watu wa Ethiopia Sahle Work Zewde,amewasili nchini Tanzania tayari kufanya ziara

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu