Dkt. Hamisi Kigwangalla awashukuru Madaktari waliomtibu.

In Kitaifa

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla amewashukuru Madaktari, wauguzi na wafanyakazi wa hospitali ya Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) ya jijini Arusha ,kwa huduma na matibabu waliyoyatoa kwake na kwa wasaidizi wake alipopata ajali mbaya ya gari Agosti 4, 2018, katika eneo la Magugu mkoani  Manyara.

Dk. Kigwangalla ametoa shukrani hizo wakati akizungumza na Madaktari, Wauguzi na wafanyakazi wa hospitali ya Arusha Lutheran Medical Centre, jijini Arusha.

Akiwa ameambatana na mkewe Dk. Bayoum Awadh, amewashukuru na kuwapongeza madaktari na wauguzi wa hospitali hiyo, kwa matibabu waliyompatia kwa kipindi chote alichokuwa hospitalini hapo na kuwaomba waendelee kuwahudumia wananchi wenye shida.

Amesema kazi ya udaktari, uuguzi na fani zote zilizo katika sekta ya afya ni za wito, na kila anayezifanya inampasa azifanye kwa wito kutoka ndani ya moyo wake.

Amesema kazi ya Udaktari na Uuguzi inafanywa na watu wachache ambao kwa kiasi kikubwa wanakua wameitika wito ama wametumwa na Mungu, na kwamba mtu yeyote hawezi kusema kuna kipato au kitu utakachoweza kumlipwa kikamtosheleza au kukidhi umuhimu na ugumu wa kazi anayoifanya.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Baraka da Prince sasa kufunga ndoa na Naj

Msanii wa Bongo fleva Baraka de Prince amebainsha wazi kufunga ndoa mwaka huu na mpenzi wake Naj. Minong’ono ilikua

Read More...

Ajibuawataka Simba watulize boli, msimu ni wao

Nyota wa Simba, Ibrahim Ajibu amesema kuwa mashabiki wa Simba watulie watakubali mziki wake kwani amejipanga kufanya maajabu. Ajibu

Read More...

Waziri Mkuu kuzindua Daftari la kudumu la kupiga kura.

Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Dkt Athumani Kihamia, amesema zoezi la uandikishaji wa daftari la Kupiga

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu