Donald Trump Junior akubali kufanyiwa mahojiano na kamati ya senate ya Marekani

In Kimataifa

Gazeti la New York Times limeripoti kuwa mwanawe Rais wa Marekani Donald Trump, Donald Trump Junior amefikia makubaliano na kamati ya ujasusi ya baraza la senate la Marekani kwa ajili ya kufanyiwa mahojiano na jopo la kamati hiyo katikati ya mwezi Juni. Likimnukuu mtu ambaye alifahamishwa kuhusiana na makubaliano hayo gazeti hilo limesema kikao hicho cha faragha kitajumuisha maswali kuhusu mada sita na kitadumu kwa chini ya saa nne. Kamati hiyo ya seneti inayoongozwa na wabunge wa chama cha Republican ilikuwa imemuita Donald Trump Junior wiki iliyopita kuhudhuria kikao hicho ili ajibu maswali kuhusiana na maafisa wa Urusi aliowasiliana nao. Ushahidi wa kwanza alioutoa Trump Junior mbele ya kamati hiyo ulikuwa kuhusu ushiriki wake katika mkutano wa mwezi Juni mwaka 2016 katika jengo la Trump Tower ambapo alikutana na raia wa Urusi waliompa taarifa kuhusu mgombea wa Urais wa chama cha Democratic wakati huo Hillary Clinton aliyekuwa anashindana na Donald Trump.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

TUME YA MADINI KWENYE MKUTANO WA KIMATAIFA WA MADINI

Kamishna wa Tume ya Madini, Profesa Abdulkarim Mruma akielezea fursa zilizopo kwenye Sekta ya Madini Tanzania katika

Read More...

Halmashauri ya Jiji la Arusha kutokomeza mimba za utotoni.

Halmashauri ya Jiji la Arusha ikishirikiana na wataalamu wa Afya kutoka mashirika mbalimbali, maafisa  elimu kata na sekondari,

Read More...

MNADA WA ALMASI WDL WAZIDI KUPAMBA MOTO.

Leo tarehe 20 Februari, 2020 mnada wa asilimia tano ya madini ya almasi kutoka katika Mgodi wa Williamson Diamond

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu