Ecowas yaingilia kati hali ya Guinea

In Kimataifa

Jumuiya ya Maendeleo ya Mataifa ya Afrika Magharibi, Ecowas, itafanya mkutano wa dharura siku ya Alhamisi kujadili hali nchini Guinea ambako jeshi limetangaza kuchukua madaraka baada ya kuipindua serikali ya Rais Alpha Konde. Mkutano huo wa viongozi wakuu wa kikanda umeitishwa siku moja tangu jumuiya hiyo ya Ecowas kulaani hatua ya jeshi kuipindua serikali nchini Guinea na kutaka kurejeshwa kwa utawala wa kikatiba au taifa hilo litawekewa vikwazo. Hayo yanajiri wakati watawala wapya wa kijeshi nchini Guinea wanajaribu kuimarisha udhibiti kwa kuamuru kikosi cha ulinzi wa rais kujiunga kwenye baraza la utawala wa kijeshi na kuwapiga marufuku maafisa wa serikali kusafiri nje ya taifa hilo. Tayari watawala hao walikwishatangaza kulivunja Bunge na kusitisha katiba ya taifa na jana walifanya mabadiliko makubwa ya kiutawala kwa kuteua magavana wapya wa majimbo nchini Guinea.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tetesi za Soka Ulaya leo Alhamisi Septemba 23, 2021

Mshambuliaji wa Arsenal na Ufaransa Alexandre Lacazette, 30, hana hamu ya kusaini kandarasi mpya klabuni hapo. Mkataba wake wa

Read More...

Wanaharakati wa haki za binadamu wahoji hukumu dhidi ya Rusesabagina

 Makundi ya kutetea haki za binadamu barani Afrika yamelalamikia uamuzi wa mahakama kuu ya Rwanda ya kumfunga jela kwa miaka 25, Paul Rusesabagina ambaye alisifika sana kwenye filamu ya Hollywood ya Hotel Rwanda.  Mahakama hiyo Jumatatu ilisema kwamba imepata Rusesabagina pamoja na washukiwa wengine 20 na hatia ya

Read More...

LISSU NA WENZAKE WAFUTIWA KESI

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeifutia kesi ya uchochezi iliyokuwa inamkabili Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleao

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu