Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania TPDC, limeanza hatua
ya awali ya utekelezaji wa mradi wa utafutaji wa mafuta katika
bonde la Mto Manonga, baada ya utafiti wa awali kubaini
uwepo wa miamba yenye viashiria vya mafuta katika bonde la
mto huo.
Mradi huo ujulikanao kama Eyasi-Wembele unatatekelezwa
katika Mikoa ambayo Mto huo unapitia ikiwemo Bonde la Ziwa
Eyasi na Bonde la Mto Manonga unaopatikana katika Mikoa ya
Tabora, Shinyanga, Singida na Manyara.
Mtaalam Mshauri wa Mradi huo Dkt Allan Mzengi kutoka TPDC, amezungumzia
uvumbuzi huo.