Familia Ya Mo Dewji Yatangaza mkwanja wa Bilioni 1 (1,000,000,000) kumpata Mo.

In Kitaifa
Familia ya Mfanyabiashara wa Tanzania Mohammed Dewji imetangaza zawadi nono ya TSH. BILIONI MOJA (1,000,000,000)  kwa yeyote atakaetoa taarifa muhimu zitakazofanikisha kupatikana kwa Mfanyabiashara huyo alietekwa.
Dau hilo limetangazwa leo October 15, 2018  na msemaji wa familiahiyo , Azim Dewji,  katika  mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za MeTL zilizopo jengo la Golden Jubilee, Posta jijini Dar es Salaam.

Familia imesema Mwenye taarifa anaweza kuwasiliana na mwanafamilia Murtaza Dewji kwa namba 0755030014, 0717208478 na 0784783228 na findmo@metl.net

“Familia inaahidi kwamba Mtoa taarifa pamoja na Taarifa vitabaki kuwa ni siri kubwa baina ya Mtoa taarifa na familia” -Amesema

Mo Dewji alitekwa na watu wasiojulikana  Alfajiri ya Alhamisi Oktoba 11, 2018 katika Hoteli ya Collosseum jijini Dar es Salaam alipokuwa amekwenda kwa lengo la kufanya mazoezi.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Suzan Kiwanga afukuzwa Bungeni.

Spika wa Bunge, Job Ndugai jana alimtoa nje ya bunge, Mbunge wa Mlimba, Suzan Kiwanga (Chadema) na kumtaka kutohudhuria

Read More...

Mtolea ajivua Uanachama wa CUF Akiwa Ndani ya Bunge Leo.

Mbunge wa Temeke Abdallah Mtolea, kwa tiketi ya CUF ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge na nafasi zote ndani

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu