Fatma Karume na Mtoto wa Chacha Wangwe kufungua Kesi 10 Ikiwemo ya kupinga Wakurugenzi kusimamia Uchaguzi.

In Kitaifa
TAASISI tatu zinazojihusisha na utetezi wa sheria na haki za binadamu, zitafungua jumla ya kesi 10 ndani ya miezi mitatu katika Mahakama Kuu ya Tanzania, kupinga zilichodai sheria kandamizi zinazominya demokrasia na uhuru wa kujieleza.
Taasisi hizo ni Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC).
Baadhi ya sheria ambazo zimeanza kupambana nazo kwa kufungua kesi ili zifanyiwe marekebisho, zimesema, ni Sheria ya Vyama vya Siasa, Sheria ya Jeshi la Polisi na Sheria ya Uchaguzi.
Wakizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, viongozi wa taasisi hizo walisema tayari wameshafungua kesi mbili katika Mahakama Kuu na kwamba kesi nane zitafunguliwa baada ya miezi miwili.
Walisema kesi hizo zimefunguliwa na wapiga kura wawili, Bob Chacha Wangwe na Allan Bhujo watakaowakilishwa na mawakili kutoka taasisi hizo tatu.
“Tayari tumeshafungua kesi mbili katika mahakama kuu, na kesi zingine nane tutazifungua miezi miwili ijayo na kufanya jumla ya kesi kuwa 10,” alisema Fatma Karume kutoka TLS.
Akizungumza katika mkutano huo, Karume alisema wamejiandaa kuzipinga sheria hizo alizoziita kandamizi, kwa mustakabali wa Watanzania.
“Hatutakata tamaa kwenye hili,” alisema Karume. “Tumeshuhudia vitendo vingi ndani ya nchi vinavyowanyima wananchi demokrasia na uhuru wa kujieleza.
“Hii ni kinyume na katiba na ndiyo maana tumeunganika kupinga sheria hizo kwa mustakabali wa taifa.”
Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa LHRC, Anna Henga, alisema haki ya kukusanyika, kujieleza ni haki ya kila Mtanzania.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu