Fayulu atishia kutangaza matokeo yake ya uchaguzi

In Kimataifa

Mgombea wa urais kupitia muungano wa upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Martin Fayulu amesema muungano huo utatangaza matokeo yake ya uchaguzi wa urais wa Desemba 30, iwapo tume ya taifa ya uchaguzi, CENI, haitotangaza matokeo yanayoendana na maamuzi ya wananchi. Fayulu ameliambia shirika la habari la AP kwamba matokeo hayo yanacheleweshwa ili wafiche ukweli. Ameionya tume ya uchaguzi ya Kongo kutocheza mchezo wowote ule utakaokuwa wa hatari. Kiongozi mwingine wa upinzani, Felix Tshisekedi na mgombea wa chama tawala, Emmanuel Ramazani Shadary, tayari wameshajitangazia ushindi, ingawa sheria inasema tume ya uchaguzi pekee ndiyo ina mamlaka ya kutangaza matokeo. Siku ya Jumapili, CENI iliahirisha kutangaza matokeo ya uchaguzi kwa wiki moja zaidi. Wakati huo huo, polisi wa kutuliza ghasia wamekusanyika nje ya tume ya uchaguzi wa Kongo, wakati nchi hiyo ikisubiri kutangazwa matokeo hayo ya uchaguzi.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Majeshi ya Marekani yauwa raia Somalia

Majeshi ya Marekani yanayoendesha mashambulizi ya angani nchini Somalia dhidi ya ngome za wapiganaji wa Al Shabab nchini humo

Read More...

Idai yapoteza makazi ya watu 400,000.

Shirika la Msalaba Mwekundu linakadiria kuwa watu 400,000 wamepoteza makaazi yao nchini Msumbiji kutokana na Kimbunga Idai kilichoipiga nchi

Read More...

Baa la njaa kuikumba Kenya.

Zaidi ya watu milioni 1.5 nchini Kenya wako katika hatari ya kukabiliwa na baa la njaa kufuatia kutokuwepo kwa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu