Gari la mafuta laua 13 Kenya

In Kimataifa

Watu wapatao 13 wamefariki baada ya tangi la mafuta ya petroli kulipuka huko magharibi mwa Kenya, usiku wa kuamkia Jumapili.

Ajali hiyo imeripotiwa kutokea wakati dereva alipojaribu kupishana na lori lingine katika barabara ya Kisumu na Busia.

Watu hao walikimbilia eneo la tukio wakiwa na madumu ya kujimiminia mafuta wakati lori hilo lilipopinduka lakini ghafla likawaka moto.

Watu wapatao 11 wakiwemo watoto, wapo hospitalini wakiwa na hali mbaya baada ya kuungua.

Iliwachukua saa mbili kwa kikosi cha zima moto kufika katika eneo la tukio karibu na mji wa Malanga katika kaunti ya Siaya yapata kilomita 315(195 miles) kaskazini-magharibi mwa mji mkuu wa Nairobi.

“Hatukuweza kupata kituo za kuzima moto kaunti ya Siaya kwa kuwa ni Nairobi,” afisa polisi Moreso Chacha alisema.

Vikosi wa kuzima moto walitokea katika kaunti za jirani , alisema.

Lori lilikuwa limebeba maziwa kutoka Busia, karibu na mpaka wa Uganda kuelekea Kisumu wakati lilipogongana na lori la mafuta lililokuwa linaelekea eneo tofauti, kamanda wa polisi amesema.

Ajali za barabarani si jambo geni katika mataifa ya Afrika Mashariki , ambapo malori na magari mengine yanapogongana kutokana sababu mbalimbali ikiwemo ya mwendo kasi.

Watu wapatao 3,000 ufariki kutokana na ajali za barabarani ,kila mwaka nchini Kenya.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu