Ghasia zamrejesha nyumbani Rais wa Afrika ya kusini.

In Kimataifa

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, amekatisha safari yake ya kushiriki kwenye Mkutano wa Jumuiya ya Madola nchini Uingereza ili kukabiliana na maandamano na ghasia zilizolikumba Jimbo la Kaskazini Magharibi mwa nchini hiyo.

Katika mkutano huo, Rais Ramaphosa alitumia muda wake mwingi kujaribu kuwashawishi baadhi ya wajumbe wa mkutano huo kuwekeza nchini mwake, huku ikiwa ni safari yake yake ya kwanza ya kimataifa baada ya kutwaa madaraka hayo kutoka kwa rais mstaafu Jacob Zuma mwezi Februari mwaka huu.

Rais Ramaphosa amerejea nchini kwake kutokana na kuongezeka kwa ghasia na maandamano yanayodaiwa fursa za ajira, makazi pamoja na kuitaka serikali kukomesha rushwa inayodaiwa kukithiri nchini humo.

Ghasia hizo zimesababisha barabara kufungwa, magari kuchomwa moto na maduka yanavunjwa hovyo huku wakazi wa eneo hilo wakimtaka kiongozi wa jimbo hilo kujiuzulu.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu