Goodbless Lema ametoa shukrani zake kwa Mbunge, Lazaro Nyalandu

In Kitaifa

Mbunge wa Arusha Mjini,  Goodbless Lema ametoa shukrani zake kwa Mbunge, Lazaro Nyalandu kwa kufanikisha safari ya Marekani ya watoto  watatu, ambao walinusurika kifo katika ajali ya basi la shule ya Lucky Vicent iliyotokea Karatu na kusababisha vifo vya watu 35

Lema amesema tangu kutokea kwa Ajali hiyo mbunge huyo amekuwa akionesha ushirikiano mkubwa jambo ambalo linastahili kupongezwa.

Aidha, tangu itokee ajali hiyo, Nyalandu amekuwa bega kwa bega na kufuatilia kila hatua, ili kuhakikisha watoto hao pamoja na wazazi wao na daktari wanasafiri kwenda nchini Marekani kwa ajili ya kupata matibabu zaidi.

Katika hatua nyingine, Nyalandu ameomba pesa zitakazo endelea kuchangwa na Watanzania na watu wengine duniani kwa ajili ya watoto hao zitumike kujenga ICU katika hospitali ya Mount Meru ambayo itakuwa ni msaada mkubwa kwa wakazi wa Arusha na mikoa jirani pindi linapotokea tatizo kama hilo.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu