Habinder Seth aandika barua kwa DPP kukiri makosa yake.

In Kitaifa

Habinder Seth, anayekabiliwa na makosa ya Uhujumu Uchumi amemuandikia barua Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) kukiri makosa yake na kuomba msamaha.

Hayo yameelezwa na Wakili wa Seth, – Michael Ngalo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyopo jijini Dar es salaam mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, – Huruma Shahidi wakati kesi hiyo ilipotajwa.

Seth, ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya PAP pamoja na James Rugemalira ambaye ni Mkurugenzi wa VIP, wanakabiliwa na mashtaka 12 wanayodaiwa kuyatenda jijini Dar es salaam na katika nchi za Afrika Kusini, Kenya na India.

Miongoni mwa mashtaka hayo ni kula njama, kujihusisha na mtandao wa uhalifu , kughushi na kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kutakatisha fedha na kusababisha hasara ya Mabilioni ya fedha.

Washtakiwa hao walifikishwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Juni 19 mwaka 2017 na hadi sasa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Katika maelezo yake, Ngalo ameuomba upande wa mashtaka kuwasaidia kwa kuwa upelelezi wa kesi hiyo umechukua muda mrefu, waelezwe ni lini utakamilika.

Baada ya maelezo ya Ngalo, Wakili wa Serikali, Wankyo Simon ameeleza kuwa wamepokea barua ya Seth, wanaifanyia kazi na majibu yatatolewa.

Kuhusu upelelezi wa kesi hiyo, Wankyo amesema bado haujakamilika na hawezi kuahidi utakamilika lini.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 24 mwaka huu.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Kipchoge anatarija kupokea taji la BBC la mwanaspoti bora

Mfalme wa mbio za Marathon Eliud Kipchoge anatarija kupokea taji la BBC la mwanaspoti bora wa mwaka rasmi

Read More...

Jerry Muro akabidhi kituo cha kisasa kwa ajili ya ukaguzi wa magari ya utali

Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Cornel Muro amekabidhi kituo cha kisasa kwa ajili ya ukaguzi wa magari

Read More...

RANCHI YA MISSENYI YATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO KWA KUIMARISHA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZILIZOPO.

RANCHI YA MISSENYI YATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO KWA KUIMARISHA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZILIZOPO. Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Ranchi za

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu