Halmashauri ya Jiji la Arusha kutokomeza mimba za utotoni.

In Afya

Halmashauri ya Jiji la Arusha ikishirikiana na wataalamu wa Afya kutoka mashirika mbalimbali, maafisa  elimu kata na sekondari, wameandaa kampeni maalumu kwa shule za sekondari zilizopo jijini Arusha, kwa kutoa, elimu ya afya ya uzazi kwa watoto wa kike na kutokomeza mimba za utotoni


Akizungumza na vyombo vya habari wakati walipotembelea shule ya sekondar Sinon afisa elimu kata ya kati katibu wa maafisa elimu katika halmashauri ya jiji la Arusha Yusta Njau amesema mkakati huo umekuja bara baada ya kutambua watoto wa kike wanapata changamoto ya kutojua afya ya uzaziInsert Yusta Njau,,,,,,,,
Kwa upande wake makamu mkuu wa shule ya sekondary Sinon mwl Sophia Alphonce  Amesema ujio huo ni mzuri kwani wanajali afya za watoto na itaboresha afya zao ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo mzuri katika masomo yao
Pia amewataka wazazi kuwa na mazoea ya kuhudhuria kwenye vikao vya shule ikiwa ni pamoja na kukaa karibu na watoto wao ili kuweza kuwapa elimu ya uzazi 


Badhi ya wadau wa afya  walioshiriki katika kutoa elimu hito wamesema kuwa elimu hiyo imesaidia kwa kiwango kikubwa kuwapa watoto wa kike ujasiri wa kujiamini na kufanya maamuz yaliyo sahihiInsert wadau….
Nao Baadhi ya wanafunzi wa kike waliopata elimu ya uzazi wameahidi kuifanyia kazi na kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza ndoto zao na kuepukana na mimba za utotoni
Hata hivyo mpango huo umeanza hivi karibuni ambapo shule zilizofikiwa ni Arusha day, Arusha Sekondary, Sombetini, Sinoni, Kaloleni, na Mrisho gambo

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WAGONJWA WA CORONA WAFIKIA 13 TANZANIA

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema idadi ya wagonjwa wa corona imefikia 13 ambapo kati yao 8 ni

Read More...

CORONA HAITAZUIA KUFANJIKA KWA UCHAGUZI – JPM

Rais Dkt. John Pombe Magufuli, amesema Ugonjwa wa Corona hautaizuia Tanzania kufanya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu. Rais

Read More...

Mshtakiwa wa mauaji ya mfanyakazi wake wa Ndani, apandishwa kizimbani

Mshtakiwa wa mauaji ya mfanyakazi wake wa Ndani Mkami Shirima(30)Mkazi wa Sakina Arusha amefikishwa tena katika mahakama ya hakimu

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu