HAMASA YA LOWASSA YAIPA STARS USHINDI

In Michezo

Anaandika Semio Sonyo moja kati ya Mwandishi wa habari na Mtangazaji nchini Tanzania mwenye mapenzi na Timu ya Taifa Taifa Stars.

Dunia ilizoea kumsikia katika medani za kisiasa, hapa namzungumzia Waziri Mkuu mstaafu Mh Edward Lowassa ambae ni moja kati ya viongozi wakubwa nchini Tanzania ambao ni nadra kuwasikia katika medani za Michezo.

Mh Edward Lowassa ni moja kati ya waliotoa hamasa kubwa kwa timu yetu ya Taifa,Taifa Stars dhidi ya Cape Verde ambae hatimae matunda ya hamasa ya kuwataka wachezaji wa Stars kuwa kama Morani wa Kimaasai yametimia baada ya Taifa Stars kuwanyuka Cape Verde jumla ya Goli 2 kwa 0 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Kama hukusikia au kuona Kauli ya Mh Edward Lowassa hiki ndicho alichokisema:

“Kule kwetu masaini tuna vijana shupavu wanaitwa Morgni.

Morani wale wanaua Simba na ni wakali kwelikweli sasa hawa wachezaji wetu wageuke kuwa Morani pale uwanjani.

Kipigo walichokipata kule kwao(Cape
Verde) iwe kama Simba amevamia zizi letu la ng’ombe wamtoe na kumuua hapana kuwa legelege” Amesema Lowassa.

Hamasa kama hizi ni miongoni mwa vitu au kauli zinazotia moyo haswa katika mapambano ya kitu chochote.

Nashauri viongozi mbalimbali wa nchi na hata wastaafu katika kila sekta michezo ni muhimu hivyo basi mkiwa mstari wa mbele kutoa sapoti katika timu ya Taifa itasaidia kuwapa ari kubwa wachezaji wetu na kupata matokeo chanya kama tulivyoona leo uwanja wa Taifa.

Tusimuachie tuu Waziri mwenye dhamana ya Michezo Mh Harrison Mwakyembe apambane na Timu ya Taifa kila Mtanzania,Kiongozi na Wananchi kwa Ujumla tuungane Pamoja kuisapoti timu yetu ya Taifa na Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania TFF.

Nimalize kumshukuru tena Mh Edward Lowassa kwa hamasa aliyoitoa kwa timu yetu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars na Viongozi wengine tujitokeze sasa kutoa hamasa kwa Timu yetu.

MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU IBARIKI TAIFA STARS TUZIDI KUSONGA MBELE DAIMA.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

TUME YA MADINI KWENYE MKUTANO WA KIMATAIFA WA MADINI

Kamishna wa Tume ya Madini, Profesa Abdulkarim Mruma akielezea fursa zilizopo kwenye Sekta ya Madini Tanzania katika

Read More...

Halmashauri ya Jiji la Arusha kutokomeza mimba za utotoni.

Halmashauri ya Jiji la Arusha ikishirikiana na wataalamu wa Afya kutoka mashirika mbalimbali, maafisa  elimu kata na sekondari,

Read More...

MNADA WA ALMASI WDL WAZIDI KUPAMBA MOTO.

Leo tarehe 20 Februari, 2020 mnada wa asilimia tano ya madini ya almasi kutoka katika Mgodi wa Williamson Diamond

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu