Hii Hapa Hali ya Mfumuko wa Bei kwa Mwezi Januari.

In Kitaifa

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Januari, 2018 umeendelea kubaki palepale asilimia 4.0 kama ilivyokuwa mwezi Disemba, 2017.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2018 imekuwa sawa na kasi ilivyokuwakwa mwaka ulioishia mwezi desemba, 2017.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu amesema kuendelea kubaki palepale kwa Mfumuko wa Bei wa mwezi Januari, 2018 kumechangiwa na bei za baadhi ya bidhaa za vyakula kutobadilika.

“Baadhi ya bei za vyakula zilizochangia mfumuko wa bei kubaki asilimia 4.0 kati ya mwezi Januari 2017 na Januari 2018 ni pamoja na mahindi kwa asilimia 8.0, maharage kwa asilimia 4.3, samaki kwa asilimia 9.0 na ndizi za kupika asilimia 9.0”, alisema Bw. Kwesigabo.

Aidha Kwesigabo aliongeza kuwa baadhi ya bei za bidhaa zisizo za chakula zilizochangia mfumuko wa bei kwa mwezi Januari, 2018 kubaki palepale ni pamoja na sare za shule kwa asilimia 2.3, huduma za afya katika hospitali binafsi asilimia 10.0, mkaa asilimia 9.4, vitabu vya shule asilimia 2.7 pamoja na gharama za malazi kwa asilimia 3.2.

Vilevile Kwesigabo alisema kuwa kwa upande wa mfumuko wa bei usiohusisha vyakula na nishati kwa mwezi Januari, 2018 umeongezeka kidogo hadi kufikia asilimia 1.4 kutoka asilimia 1.3 kama ilivyokuwa mwezi Desemba 2017.

Kwesigabo aliongeza kuwa mfumuko wa bei nchini una mwelekeo unaofanana na baadhi ya nchi nyingine za Afrika Mashariki ambapo nchini Uganda mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2018 umepungua hadi asilimia 3.0 toka asilimia 3.3 kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba 2017 na kwa upande wa Kenya kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2018 umeongezeka hadi asilimia 4.83 toka asilimia 4.50 kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba 2017.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu