Huzuni zatamalaki mazishi ya Bilago-Buyungu.

In Kitaifa

Mazishi ya mwili wa aliyekuwa mbunge wa Buyungu (Chadema), Kasuku Samson Bilago ulizikwa jana katika makaburi ya Kijiji cha Kasuga wilayani Kakonko, mkoani Kigoma alipozaliwa.

 

Shughuli ya mazishi hayo ilianza kwa ibada ya misa ya mazishi katika Kanisa Katoliki Kigango cha Kasuga na kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu kabla ya kuelekea makaburini kwa maziko.

 

 

Wakati wa shughuli hiyo, vilio, simanzi na majonzi vilitawala kwa wakazi wa Kasuga, ndugu, marafiki,  wanachama na wafuasi wa Chadema wakati mwili huo ulipowasilishwa kanisani na baadaye kupelekwa makaburini.

 

 

Waliopata nafasi ya kumzungumzia Bilago, wengi wao walisema marehemu alikuwa akiishi maisha ya kijamaa na wananchi wa jimbo lake la Buyungu na kila sehemu aliyofanya kazi ikiwemo bungeni na fani yake ya ualimu.

Bilago aliwahi kuwa mwalimu na baadaye Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) katika mikoa ya Kigoma, Rukwa na Mbeya kabla ya kuingia kwenye siasa.

 

Bilago ambaye pia alikuwa ni Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Magharibi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho, alifariki dunia Jumamosi iliyopita, Mei 26, 2017 mchana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wakati akipatiwa matibabu

Bilago alizaliwa Februari 2, 1964 na alikuwa mwanachama wa cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Alichaguliwa kuwa mbunge wa Buyungu kuanzia mwaka 2015 hadi mauti yalipomkuta.

 

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu