Idadi ya vifo vya virusi vya corona yaongezeka Uhispania

In Kimataifa

Idadi ya vifo nchini Uhispania kutokana na virusi vya corona imepanda kwa zaidi ya watu 700 leo, na kuipiku China na sasa ni nchi ya pili baada ya Italia kwa kurekodi idadi kubwa ya vifo, wakati janga hilo likisambaa kwa kasi barani Ulaya. Uhispania imerekodi vifo vya watu 738 vilivyotokea leo, na kufikisha jumla ya 3, 434 ikiwa ni zaidi ya China ambayo in vifo 3,285. Fernando Simón, ni mkurugenzi wa kituo cha uratibu wa majanga ya dharura katika wizara ya Afya nchini UhispaniaNchini India, taifa kubwa kabisa duniani, serikali imewafungia majumbani raia wake bilioni 1.3, wakati nchini Marekani, wabunge wameidhinisha mpango mkubwa wa msaada wa ndani wa trilioni 2. Nchini Uingereza, Mwanamfalme Charles ambaye ana umri wa miaka 71, ameambukizwa virusi hivyo. Italia ndilo taifa lililoathirika zaidi Ulaya, likiwa na zaidi ya maambukizi 69,000 na vifo 6,800. Bunge la Ujerumani limeidhinisha hatua za kuiwezesha serikali kutoa msaada wa zaidi ya euro trilioni moja kuwasaidia raia wake milioni 83

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WAGONJWA WA CORONA WAFIKIA 13 TANZANIA

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema idadi ya wagonjwa wa corona imefikia 13 ambapo kati yao 8 ni

Read More...

CORONA HAITAZUIA KUFANJIKA KWA UCHAGUZI – JPM

Rais Dkt. John Pombe Magufuli, amesema Ugonjwa wa Corona hautaizuia Tanzania kufanya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu. Rais

Read More...

NEC yakutana na vyama vya siasa.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi hapa nchini NEC Jaji Kaijage ametangaza awamu ya pili ya uboreshaji

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu