IMF yaionya Tanzania juu ya kupungua kwa kasi ya ukuaji wa uchumi.

In Kitaifa, Uchumi
Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ijumaa hii limeonya kuhusu kupungua kwa kasi ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania, likisema kuwa serikali inafaa kuchukua hatua za haraka ili kubadilisha mwelekeo wa kushuka.
Katika taarifa yake mpya kuhusu uchumi wa Tanzania, IMF imesema kuwa, licha ya kuwa takwimu za pato la taifa kuoyesha kukua, lakini takwimu ningine za uchumi zinaeleza kudorora kwa shughuli za kiuchumi. Taarifa hiyo imetolewa baada ya kukamilisha mapitio yake ya Sera za Kukuza Uchumi PSI kuhusu Tanzania.
Ukusanyaji wa mapato umekuwa mdogo kuliko ulivyotarajiwa na ongezeko la alama za imani limekwama katika baadhi ya mabenki kutokana na kuongezeka kwa mikopo mibaya.
Kumekuwa na athari mbaya kwenye ukuaji wa uchumi katika kipindi kifupi kutokana na utekelezaji mdogo wa bajeti, ulioleta changamoto kwenye mazingira ya kibiashara, na sekta binafsi ikilalamika kubanwa sana na sheria.
Uchumi wa Tanzania katika kipindi cha muongo mmoja uliopita ulikuwa unakua kwa asilimia 7 kwa mwaka, lakini mwezi Novemba Benki ya dunia ilitangaza kuwa kasi hiyo huenda ikapungua hadi asilimia 6.6 mwaka jana

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

IGP Sirro akutana na Rais wa TLS Fatma Karume.

   IGP Simon Sirro amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Fatma Karume aliyefika Makao Makuu ya

Read More...

Magereza watoa ufafanuzi kuhusu Sugu.

Jeshi la Magereza nchini limetoa ufafanuzi kuhusu uamuzi wa mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph ‘Sugu’ Mbilinyi kuendelea kuvaa nembo

Read More...

Watu 104 wahukumiwa kifungo cha maisha Uturuki.

Mahakama ya mjini Izmir nchini Uturuki imetoa adhabu kali ya kifungo cha maisha kwa washtakiwa 104 waliopatikana na hatia

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu